Wednesday 23 December 2015

WAZIRI UMMY MWALIMU AANZISHA "MPISHE MZEE KWANZA APATE HUDUMA"

IMG-20151222-WA0027
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Tanga, wakati akitoa mwelekeo wa vipaumbele vyake kwa wazee wa Tanzania kupitia kwa wazee wa mkoa wa Tanga.
IMG-20151222-WA0028
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya nchini, kuweka anuniani inayosema"Mpishe mzee kwanza apate huduma".
Ametaka maneno hayo kuandikwa kwenye dirisha la mapokezi, vyumba vya madaktari na sehemu ya dawa.
Agizo hilo amesema linakwenda sambamba na uwepo wa madirisha ya wazee katika vituo vyote vya serikali vya kutolea huduma za afya.
Mhe Ummy pia ameahidi kupeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Taifa ya Wazee katika Bunge ili kuhakikisha haki na stahili za wazee nchini zinatekelezwa kikamilifu.
Wazee walieleza kero zao kubwa ni kupata matibabu, kutokuwa na kipato cha uhakika na vitendo vya kudharauliwa na jamii.
Kauli ya Waziri huyo ilitolewa katika mkutano wake alioufanya katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Tanga.
Katika mkutano huo ambapo alikutana na wazee wa Tanga wakiwakilisha wenzao wa Tanzania aliuutisha ili kutoa mwelekeo wa vipaumbele vya serikali ya awamu ya tano kwa wazee wa Tanzania.
Vipaumbele hivyo ni pamoja na bima ya afya ili kupata matibabu ya uhakika na kuhakikisha sheria ya Taifa ya Wazee inapitishwa na Bunge ili kuwezesha wazee kufaidi haki na stahili zao ikiwemo kupata pensheni zitakazowawezesha kuendelea na maisha yao bila shaka.
IMG-20151222-WA0026
Wazee wa mkoa wa Tanga wakiuliza wakitoa maoni na kumshukuru Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) kwa kuonyesha upendo wa kuwajali katika kuboresha huduma za afya kwa wazee wakati mkutano wake na wazee wa mkoa huo.
IMG-20151222-WA0024
IMG-20151222-WA0025
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipokea risala iliyosomwa kwa niaba ya wazee wa mkoa wa Tanga.
IMG-20151222-WA0021
Pichani juu na chini ni baadhi ya wazee wa mkoa wa Tanga waliohudhuria mkutano ulioitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
IMG-20151222-WA0022
 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA