Saturday 12 December 2015

ZIJUE DALILI ZA KUTODUMU NA MARAFIKI ULIONAO AU ULIOWAPOTEZA

Ulimwengu jinsi ulivyo, hupati picha kama binadamu angekuwa mmoja angeishi vipi peke yake.
Kwani ukiangalia mfumo ulivyo, unamfanya na kumtaka binadamu awategemee wenzake katika kutimiza mahitaji yake, kuanzia kimwili hadi kihisia.
Hali hiyo humfanya kila binadamu awe tegemezi kwa binadamu wengine, katika kukamilisha furaha  yake ya kila siku.

Lakini kwa kuwa watu unaokutana nao hamfanani tabia kuna kipindi lazima kutatokea utengano na hao marafiki.Ama uwe wewe umechoka na mwenendo wao au wao wachoke na mwenendo wako.

Lakini mpaka utengano kukamilika,  kuna dalili huwa zinajionyesha mwanzoni ambazo ukizisoma utagundua mapema sana kwamba kuna kitu unatakiwa ufanye ama kuuokoa au kuumaliza kabisa na wewe.

Hebu tuangalie dalili 5 unazoweza kuziangalia katika urafiki wako:

1.MUONEKANO WA USONI

Kama wana nyuso za furaha wanapokuona  hapo jua wanafurahia uwepo wako.
Lakini ukiona umetokea tu nyuso za watu zimebadilika ujue hizo ni dalili za kuwa uwepo wako hauna umuhimu kwao.

2.MATEMBEZINI

Kama wanakuita katika safari zao za matembezi ya kawaida ujue wanapenda uwepo wako lakini kama kila siku unashtukia tu wanahadithiana waliyoyafanya jana ambapo wewe hukuwepo hiyo ni dalili mbaya.

3.KUKUPIGIA SIMU AU KUKUTUMIA MESEJI

Kama ukiona wewe haupigiwi wala kutumiwa meseji kama kipindi cha nyuma huku wao
wanawasiliana ujue dalili sio nzuri.

4.MANENO KUTOKA KWA MARAFIKI ZAO

Hata marafiki zako pia nao wana marafiki, kwahiyo endapo hawafurahii uwepo wako wao ndio wa kwanza kuwasimulia habari zako wasizozipenda.

5.KUKUPINGA KILA UNACHOONGEA

Yaani mkiwa mna jadili jambo,  wao ndio huwa wa kwanza kukucheka unachoongea.
Wanakuonyesha wazi kuwa,  hawakubaliani na unayoongea hata kama kuna ukweli ndani yake.

KUPOTEZA MARAFIKI KATIKA MAISHA YETU SI KITU KIZURI.

USIPOTAFUTA TATIZO LIKO KWAKO AU KWAO UTAJIKUTA HAUDUMU NA MARAFIKI KAMWE. 

KAMA UKIONA URAFIKI HAUNA FAIDA UMALIZE 
LAKINI  UKIONA UNAFAIDA.PIGANIA KUUDUMISHA KWA KUREKEBISHA KASORO ZILIZOPO.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA