WEEKEND VIBES::::ACHA HARAKA, JIFUNZE KUSUBIRI
Ni jambo la kumshukuru Mungu
kwamba tumekuwa miongoni mwa waliochaguliwa kuuona mwezi huu, ingawa
yatupasa tuombe sana ili mwaka huu uwe wa baraka kwetu. Maana mnajua kwa kiasi gani wapendwa
wetu walivyopotea na hatutawaona tena.
Leo nikwa ofisini nilikuwa natafakari stori kadhaa za washkaji wanaolaumu kupigwa mizinga na "mademu" zao, halafu nikwaza wakati fulani kuna mabinti wakati tukipiga stori walisema kuwa wanaume tuna haraka sana ya tendo hata kabla uhusiano haujakomaa, haha nakumbuka yule mdada alisema "Mhmhm jamani mtu hata wiki haijaisha kisa nimemkubali ndio anataka tuanze kuminyana ,aisee mimi sipendi kabisa"........ Hapa jibu moja tu limepita kichwani, SUBIRA...
Mada
yangu leo kama unavyoweza kuiona hapo juu kwenye kichwa cha
habari, inawazungumzia zaidi akina dada, kwa sababu zilizo wazi kabisa
kwamba, wao ndiyo maua ya dunia, bila wenyewe hata maisha sijui
yangekuwaje ,lakini sijasahau kaka zangu kwani sote tunategemeana.
Ni
jambo la kweli kwamba mara nyingi wanaume ndiyo wanaokuwa wa kwanza
kutangaza nia kwa mwanamke tofauti na inavyokuwa kinyume chake.
Inapotokea mwanamke ‘anamtokea’ mwanaume, huwa ni gumzo na siyo ajabu
kukuta mwanaume akikataa, anaona kama vile anategewa au mwanamke
anayemtongoza ana kasoro.
Kwa
wanaume, wengi wao hupenda baada ya kukubaliwa katika kutongoza kwao,
kinachofuata kiwe ni tendo la ndoa na si vinginevyo wakati kwa wanawake,
baada ya kukubaliwa, wao hupenda kwanza wazoeane kwa maongezi,
vijizawadi na mitoko ya hapa na pale kabla ya kuhitimisha kwa tendo. Hii
ni hulka ambayo imeendelea hadi kujenga mazoea, kiasi kwamba wanaume
wakimpata mwanamke wa kushiriki naye tendo siku ya kwanza tu ya kukutana
kwao, huwaona kama wasiofaa. Wamezoea wakikubaliwa, wazungushwe japo
siku mbili tatu kabla ya kumalizana.
Sasa
utamu unakuja pale mwanaume baada ya kukubaliwa, kwa kawaida, atatoa
mwaliko kwa mwenzake kwa ajili ya mazungumzo, mara nyingi huwa ni
hotelini kwa ajili ya chakula cha mchana au kwa wanywaji basi hukutana
eneo zuri kwa ajili ya kujipatia mbili tatu.
Inaweza
kuwa siku ya kwanza, ya pili na pengine kwa siku kadhaa. Katika kipindi
hicho, mwanaume atakuwa ametoa ofa kama hivyo ya vinywaji, vocha na
hata pesa kwa mwenza wake. Uzoefu unaonyesha kuwa mara nyingi wakaka
wanapoulizia kuhusu faragha, hukutana na maswali au majibu kama “yaani
mbona wewe una haraka? Harakaharaka haina Baraka”.
Na
hata wengine huwaambia maneno kama “Yaani wewe hicho ndicho
unachokiwaza.” Kauli hizi za akina dada huwa na nia ya kupunguza spidi
ya jamaa wenye uchu. Kama nilivyodokeza pale juu, kwa mujibu wa mazoea
yaliyojengeka, inatarajiwa kuwa walio katika uhusiano watachukua muda
kidogo kabla ya kufikia hatua ya kushiriki tendo.
Lakini
wakati akina dada wamekuwa wakisisitiza kutokuwa na haraka ya kushiriki
tendo kwenye uhusiano mpya, uzoefu pia unaonyesha wao huwa hawasubiri
kabla ya kuanza mambo yao. Katika siku ya kwanza ya kutongozwa na
kukubali, kesho yake wataanza kuomba vocha. “Baby
naomba vocha niongee na mama, yaani nimemmiss sana,” utasikia msichana
akimwambia mpenzi wake. Baadhi hununua muda wa maongezi kweli, lakini
wengi wao hutuma hela kutegemea na uzuri wa mdada.
“Baby
naomba niongezee elfu ishirini kuna kitu nataka kununua hapa
nitakurudishia..” wengine huja na kauli kama hizi. Kifupi ni kwamba
wasichana wengi huwasumbua wenza wao wapya kwa staili kama hii. Maombi
kama haya huwafanya wanaume wahangaike sana kuwatimizia wapenzi wao,
lakini pia huwaumiza sana kisaikolojia.
“Hivi
kama huyu anaanza kupiga mizinga hata hatujafahamiana vizuri, hivi
akishakuwa mpenzi wangu si ndo balaa,” baadhi ya akina kaka hujiuliza.
Inafika mahali kama huna cha kutoa basi inabidi usugue benchi mpaka upate,,Duh !! Hii hatari sana.
Ngoja nirejee kauli yangu tena,SUBIRA. Sote tusipokuwa wavumilivu kidogo na kujenga uwezo wa kuzishinda tamaa zetu za kimwili na kifedha hakika mambo yataenda sawa .
Sikatai kwamba zawadi zisitolewe au watu msiwe na faragha lakini kila jambo linawakati wake,kama huyo mpenzi siyo wa mpito basi kila hatua ipigwe kwa wakati sahihi Ukiona ana haraka sana SHTUKHAAAA!!!!!!.
Ifike mahali Pesa na zawadi visiwe mtihani kwa mwanaume ili avune pendo na vile vile ngono isiwe mtihani kwa mwanamke ili apate pesa na zawadi.
Kwa maoni na ushauri tuwasiliane - Dickson Mulashani -(KD MULA)
0 comments:
Post a Comment