MAALIM SEIF ASEMA KUWA HATAKUBALI UCHAGUZI KURUDIWA
KATIBU Mkuu wa Chama
cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana amezungumza na wahariri wa vyombo
vya habari juu ya Mustakabali wa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na hatua
ambayo imefikiwa hadi hivi sasa.
Maalim anasema tume
haina mamlaka ya kutengua matokeo bali ina mamlaka ya kurudia kuhesabu kura.
Mwenyekiti wa tume Zanzibar alienda kinyume cha katiba kwa kufanya maamuzi bila
kushirikiana na tume. Maalim anasema Katiba inasema "kila uamuzi wa tume
ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi". Anasema katiba imetumia
neno 'Lazima' na mwenyekiti kwenda kinyume inafaa kuchukuliwa hatua.
Pia Maalim Seif
Sharif Hamad amemtaka rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe
Magufuli kuongoza mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani
Zanzibar kwa kufuata misingi ya kikatiba na sheria baada ya mazungumzo
yaliyokuwa yanaendelea na Dr Ali Mohamed Shein wa CCM kwa kuwashirikisha marais
wastaafu wa Zanzibar kutoonesha kuzaa matunda.
0 comments:
Post a Comment