MAKABURI MATANO YAGUNDULIWA BUJUMBURA
Raia wa Burundi wakishanga kaburi
Shirika
la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International
limesema limeena picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa
Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi.
Amnesty
limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi
yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa
Bujumbura.
Shirika
hilo linaongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao
wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya
watu waliouwawa siku ya tarehe 11,desemba,siku ambayo ilishuhudia
machafuko makubwa mjini Bujumbura.
Ripoti
hiyo imekuja siku chache kabla ya mkutano wa viongozi wa umoja wa Afrika
kukutana kujadili hatima ya mgogoro wa Burundi huko Ethiopia.
Mgogoro
wa Burundi ulianza april mwaka uliopita, wakati ambapo raisi Pierre
Nkurunzinza alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi kwa awamu ya tatu na
kuchaguliwa tena kuwa raisi mwezi july mwaka wa jana.
-BBC
0 comments:
Post a Comment