MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA IFAKARA (IFUWASA) YAUNDA MPANGO WA MAENDELEO KWA MWAKA 2014 HADI 2017
Picha toka maktaba |
Na Tadeo Jackson,Ifakara
Mamlaka ya majisafi
na usafi wa mazingira Ifakara
(IFAUWASA) Imeunda mpango wa maendeleo kwa mwaka 2014 hadi 2017 ambao utaongeza
usambazaji wa maji katika halmashauri ya mji wa Ifakara
wilayani Kilombero.
Bwana Akley Galawika ambaye ni meneja amesema kuwa malengo makuu ya
mpango huo ni kuongeza maji yanayozalishwa kwa kutumia pampu za umeme ili
kuweza kusukuma maji kutoka kwenye visima na kurahisisha upatikanaji wa maji kwa
matumizi ya kawaida,pia kuboresha uondoaji wa
maji taka katika halimashauri ya mji wa
ifakara kwa kutumia gari.
Vilevile malengo mengine ya mradi huo ni
kuboresha mtandao wa usambazaji wa maji kwa kutumia mpango wa Kiburubutu na kuhakikisha
kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ili kupunguza tatizo la uhaba wa maji.
Aidha Bwana Galawika
amesema katika halmashauri ya mji wa Ifakara kuna jumla ya visima 185 ambavyo
viko chini ya serikali, kati ya hivyo 52 ni vibovu kabisa na vinatakiwa kufanyiwa
matengenezo,na kuboresha visima vingine.
Mpango wa maendeleo
ambao uko chini ya mamlaka ya (IFAUWASA)
utaanzia Mhola na Lipangalala na utagharamu kiasi cha bilioni sita pointi saba.
0 comments:
Post a Comment