NCHI 27 KUFANYA KAMPENI DHIDI YA IS
Majeshi yanayoongozwa na Marekani wakifanya mashambulizi dhidi ya IS nchini Iraq
Mawaziri
wa ulinzi wa nchi za magharibi wanaokutana jijini Paris wamekubaliana
kuongezea nguvu zaidi kampeni dhidi ya wanamgambo wa Islamic State
nchini Iraq na Syria.
Waziri wa
ulinzi wa Uingereza, Michael Fallon, amesema kampeni hiyo ya pamoja
italenga zaidi uongozi wa IS na miundombinu(mawasiliano na njia zao za
usafirishaji).
Waziri wa
ulinzi wa Marekani, Ash Carter amesema wana nia kuu tatu ambazo ni
kuisambaratisha IS katika ngome zake za Raqqa na Mosul, kupambana na
matawi yake duniani kote na kulinda raia.
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi 27 zikiwemo Iraq na nchi kadhaa za kiarabu watakutana mjini Brussels mwezi ujao.
-BBC
0 comments:
Post a Comment