Thursday 21 January 2016

LIVERPOOL ,SPURS ZAMALIZA VIPORO NA KUSONGA MBELE KOMBE LA FA

Mshambuliaji wa Liverpool, Christian Benteke akipiga kichwa kilichoenda juu ya lango la Exeter City katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Tatu Kombe la FA England. Liverpool ilishina 3-0 usiku wa jana Uwanja wa Anfield, mabao ya Joe Allen, Sheyi Ojo na Joao Teixeira na kufuzu Raundi ya Nne, ambako itakutana na West Ham United.
The Liverpool players celebrate taking an early lead against League Two Exeter on their way to an easy victory
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na wenyeji Liverpool kivutio kikubwa kilikuwa wachezaji makinda ambao walisheheni katika kikosi hicho na kufanya mashabiki waliojaa uwanjani hapo kusahau kipigo dhidi ya Manchester United kwa kucheza soka safi na la akili zaidi.


TOTENHAM

Mshambuliaji wa kimataifa wa Korea Kusini, Son Heung-min (kushoto) akifumua shuti kuifungia Tottenham Hotspur bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wa marudiano Raundi ya Tatu Kombe la FA England Uwanja wa King Power. Bao lingine la Spurs limefungwa na Nacer Chadli na sasa itamenyana na Colchester United ugenini katika Raundi ya Nne.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA