RAIS MAGUFULI AMFARIJI MAMA MARIA NYERERE KWA KUFIWA NA MKWEWE
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole
Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere
aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa
Taifa Msasani Dar es salaam jana Januari 11,2016
Rais Magufuli akiwapa pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam jana.
Rais Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku.
Rais Magufuli katika picha ya pamoja na wanafamilia
Rais
Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake
Msasani kumfariji kufuatia kifo cha Mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere
huko Maryland, Marekani.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 11
Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama
Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana
huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema
mwezi huu.
Pamoja
na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani
Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia
wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
kuondokewa na ndugu yao.
Msemaji
wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais
Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa
marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU11 Januari, 2016
0 comments:
Post a Comment