TAKWIMU:::WATU 331 WAFARIKI DUNIA MKOANI MBEYA KWA AJALI ZA BARABARANI 2015
Jumla ya
watu 331 wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani mkoani Mbeya
katika kipindi cha mwaka 2015 ikiwa ni ongezeka la vifo 27
ikilinganishwa na vifo 304 vilivyotokea mwaka 2014.
Kamanda
wa Polisi mkoani Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Ahmed Msangi
amesema ongezeko hilo la vifo linaenda sambamba na ongezeko la makosa ya
usalama barabarani na idadi ya wahalifu wa makosa hayo.
Katika
mahojiano maalumu na Kituo Star TV, Kamanda Msangi amesema mwaka 2014
jumla ya makosa 61,466 yamepatikana wakati mwaka jana makosa yalikuwa
76,346 ikiwa ni ongezeko la makosa 14,898 ambapo kati yake mwaka 2015
makosa 71, 429 na 54,849 ya mwaka 2014 kwa pamoja yametozwa adhabu zenye
thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 3 na Milioni 203 ikiwa ni ongezeko
la Shilingi Milioni 497.4 kwa tozo za mwaka 2014.
Kuhusu
Pikipiki za miguu miwili na mitatu maarufu kama na Bajaji, Kamanda
Msangi amesema ajali zake nazo zimeongezeka kutoka 141 mwaka 2014 mpaka
159 mwaka jana ambazo kwa pamoja zimesababisha vifo 162 na kujeruhi watu
231 na kwamba nyingi zimesababishwa na uzembe wa kukosa umakini kwa
madereva.
Jiji la Mbeya lina pikipiki za miguu mitatu zaidi ya 2100 wakati pikipiki za miguu miwili ni zaidi ya 3000.GPL
0 comments:
Post a Comment