Thursday 11 February 2016

CHUO KIKUU CHA SMMUCO CHALAMBA UDHAMINI WA JEZI TOKA MARENGA INVESTMENT

Dr. Emmanuel Kileo (mwenye shati jeusi) akipokea moja kati ya jezi hizo  kulia ni Meneja masoko wa Marenga Investent Bwana Octavian
 Stefano Moshi Memorial University College kampasi ya mjini imeuanza mwaka vizuri kwa kupata udhamini wa seti moja ya jezi kwa ajili ya mpira wa miguu kutoka kwa kampuni ya Marenga Investment.
Akizungumzia sababu za udhamini huo uliogharimu kiasi cha TSHs laki nne na nusu Meneja masoko wa Marenga Investment ,Octavian amesema hii ni kudumisha na kufanya kwa vitendo kauli mbiu ya inayofahamika kaka MICHEZO NI AFYA ,FURAHA na MAHUSIANO.
Tunaamini uwepo wa vifaa vya michezo unaleta hamasa nasi kulingana na kauli mbiu yetu tunajivunia kuwa sehemu ya kuokoa vijana wengi kiafya" alisema Octavian.



Akizungumza wakati wakupokea jezi kwa niaba ya Uongozi wa Chuo ,Mchungaji , Dr. Emmanuel Kileo amewapongeza Marenga Investment kwa kuonesha kujali michezo na kuahidi ushirikiano mwema katika siku za usoni.

Kadhalika uongozi wa  serikali ya wanafunzi  wa chuo hicho ukiongozwa na Makamu wa rais Ndg.Festus Mjengi pamoja na waziri wa michezo Ndg. Moses Mwankuga haukusita kuonesha kufurahishwa na udhamini huo na kuahidi kuendeleza michezo ili kufanya vizuri katika michuano ya nje.

Huu ni udhamini wa kwanza wa vifaa vya kimichezo kwa chuo hicho kishiriki cha chuo kikuu Tumaini Makumira kwa mwaka wa masomo 2015 /2016.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA