Sunday 7 February 2016

DRC BINGWA WA CHAN 2016 , IVORY COAST YAAMBULIA MSHINDI WA TATU

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiyo mabingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee. Hiyo inafuatia kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali ya michuano ya mwaka huu Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda. Elia Meschack alifunga dakika ya 28 na 62 kabla ya Jonathan Bolingi kufunga la tatu dakika ya 73 kuifanya DRC itwae taji la pili katika fainali za nne tangu kuanzishwa kwa CHAN. Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

DRC wamerudia mafanikio ya mwaka 2009 walipotwaa ubingwa wa fainali za kwanza za CHAN nchini Ivory Coast
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Ivory Coast iliifunga mabao 2-1 Guinea na kunyakua Medali ya Shaba. Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Mohamed Youla aliyejifunga dakika ya 33 na Gbagnon Anice Badie dakika ya 35, wakati la Guinea lilifungwa na Aboubacar Leo Camara dakika ya 86.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA