FBI WAHAHA KUPATA USHAHIDI CALIFONIA
Shirika
la kijasusi nchini Marekani FBI, miezi miwili baada ya watu kumi na
wanne kuuwawa mjini Califonia na wanandoa wa kiislamu wenye itikadi
kali, wachunguzi hawajabaini ushahidi wowote katika simu iliyopatika
kutoka kwa mmoja wa wauaji.
Mkurugenzi
wa shirirka hilo la kijasusi,James Comey amekuwa akitoa ushaidi katika
kamati ya upelelezi ya seneti ya Marekani,kufuatia kupigwa kwa risasi
kwa wingi San Bernardino mwezi desemba.
Bwana
Comey anasema kuwa mawasiliano yao yalikuwa ni ya siri na waliweza
kutumia tekinolojia ya hali ya juu kuvuruga mitambo, hivyo kuathiri
sheria kuweza kuchukua mkondo wake.
Sheria ya
kuondoa ulinzi wa mawasiliano hayo bado unajadiliwa mjini Washngton ili
kukabiliana na mashambulizi yaliyotokea California.
-BBC
0 comments:
Post a Comment