Thursday, 11 February 2016

NAIBU WAZIRI WA AFISI YA MAKAMU WA RAIS TANZANIA MUUNGANO NA MAZINGIRA MHE LUHAGA MPINA AFANYA ZIARA KUTEMBELEA MIRADI YA KUHARIBIKA NA TABIA NCHI ZANZIBAR

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa na aliyekuwac Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo kwa sasa ni mgombea Jimbo la Kikwajuni Uwakilishi Mhe Nassor Salim Jazira akiwa katika ziara hiyo ya Mhe Waziri Zanzibar   
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Eng Hamad Yussuf Masauni akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Jangombe Ali Hassan Omar King wakiwa katika ziara hiyo kutembelea miradi ya Muungano ya Tabia Nchi Zanzibar. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi akitowa maelezo jinsi eneo hilo la kilimani lililoathirika na Tabia Nchi Zanzibar likiwa chini ya mradi wa Kujenga Uwezo wa Jamii Kuhimili Mabadiliko Tabia Nchi (LDCDF)kilimani kwa Upandaji wa Mikoko na Uwekaji wa Matuta kuzuiya Mmomonyoko wa Ardhi katika Ukanda wa Bahari.
Eneo ambalo limekumbwa na Tabia nchi katika kilimani likiwa limejaa maji ya pwani  
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake ya kutembelea miradi ya kuhifadhi mazingira Zanzibar akitembelea moja ya mradi huo ulioko kilimani Zanzibar kujionea jinsi ya hali ya uharabifu wa Tabia Nchi katika eneo hilo.  
Ujumbe wa Maafisa wa Mazingira wa Afisi ya Rais Muungano wakitembelea eneo hilo na Naibu Waziri Mhe Luhaga Mpina.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Masauni akiwa katika ziara hiyo kutembelea eneo hilo la kilimani lililoharibika kwa kuliwa na bahari kutokana na Tabia Nchi.  
Eneo la Ufukwe wa Kilimani uliovyoliwa na Tabia Nchi kama unavyoonekana pichani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, wakati wa ziara yake hiyo leo katika eneo la kilimani Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, wakati wa ziara yake hiyo leo katika eneo la kilimani Zanzibar. 
Sheha wa Shehia ya Kilimani akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitowa maelezo ya eneo mpja lililoathirika na Tabia nchi katika eneo la kilimani akimuonesha uliokuwa uwanja wa kilimani Stars kwa sasa uwanja huo umekuwa ni sehemu ya kukaa maji ya bahari wakati wa maji kujaa. na kufika karibu na sehemu ya makaazi ya wananchi.
Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina akitembelea eneo hilo wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya Tabianchi Zanzibar akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakiwa kastika ufukwe wa pwani ya kizingo. 
Naibu Waziri wa Afisi ya Rais Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina na Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nadi Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni wakitembelea eneo la ufukwe wa pwani ya kilimani ilioathirika kwa kuliwa na bahari sehemu kubwa ya eneo hilo na kuingia maji katika maeneo ya jirani na makaazi.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kudhibiti tabia nchi kwa eneo hilo la kilimani na kuharibu sehemu kubwa ya eneo hilo ambalo lilikuwa na uwanja wa mpira na kuliwa na bahari.
Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Joelson Mpina akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo hilo lililokubwa na athari za Tabia nchi katika pwani ya ufukwe wa kilimani na kuagiza kupandwa kwa mikoko katika eneo hilo ambolo ifikapo mwezi wa marchi na fedha zake zipo kwa kazi hiyo na zoezi hilo limeaza mwezi huo kwa kuaza kwa kupandwa kwa miti ya mikoko na ujengaji wa tuta la kuzuiya maji ya bahari kuendelea kula eneo hilo ambalo tayari limeharibia na maji ya bahari.
Naibu Waziri Afisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Joelson Mpina Naibu Waziri wa Mambi ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mbunge wa Jimbo la Jangombe Mhe. Ali Hassan Omar King wakitembelea eneo la pwani ya kilimani lililokumbwa na athari za TabiaNchi. wakati wa ziara yake Kisiwani Zanzibar kutembelea maeneo hayo.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com. 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA