SERIKALI ITAENDELEA KUWAFUNGIA MAGETI WATUMISHI
Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususani wa kipatao cha chini na wale maskinini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo.
Dkt. Kigwangalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali haitowavumilia watumishi wazembe, hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe, tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi, mtumishi akizembea tutamtumbua majipu, akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“Hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi,” alisema naibu waziri.
Hata hivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.
“natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo,” alieleza Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.
0 comments:
Post a Comment