Tuesday 16 February 2016

TANZIA:: MSANII JOHN WALKER AFARIKI DUNIA ,MUHIMBILI

John Walker enzi za uhai wake

Mwanamuziki na Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Watukutu Michael Denis maarufu  (John Walker)  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika alipokuwa akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hizi imeelezwa kuwa Michael aliumia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika paji la uso na kumwingia ndani kiasi cha nchi moja kutoka katika gari walilokuwa wakilirekebisha eneo la  Sinza.

Funguka Live imefanya mawasiliano na mmoja wa rafiki wa marehemu ambaye ni msanii wa kundi la Wagosi wa Kaya ,Fredrick Gerson Marik maarufu kama Mkoloni aliethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa msiba upo Ilala Bungoni na taarfa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya maamuzi ya familia.

 John Walker alijipatia umaarufu kutokana na upekee katika uimbaji wake ambapo aliimba kama 'mlevi' hivyo kufanya kujulikana zaidi hasa kupitia kibao chake kilichoitwa Sofia.


FUNGUKA LIVE inatoa pole kwa familia pamoja na tansia nzima ya sanaa ya muziki kwa kumpoteza "John Walker".

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA