Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo zaidi Burundi
Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa uko tayari kuiwekea vikwazo zaidi nchi ya Burundi.
Mawaziri
wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wamesema leo kuwa wako tayari
kutekeleza vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Burundi. Uamuzi huo
umechukuliwa baada ya kushindwa mazungumzo ya kukomesha mgogoro wa
kisiasa wa Burundi ambao umesababisha mauaji ya watu zaidi ya 400.
Taarifa
iliyotolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels
imesema kuwa umoja huo uko tayari kuchukua hatua za kukabiliana na watu
wanaohusika na harakati za ukatili, ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa
haki za binadamu.
Mwaka
jana Umoja wa Ulaya ulianza kutekeleza baadhi ya vikwazo dhidi ya
Burundi ikiwa ni pamoja na kuwapiga marufuku ya kufanya safari katika
nchi za Ulaya maafisa wanne wa serikali ya Bujumbura walio karibu na
Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo. Waafisa hao walituhumiwa kutumia
vibaya madaraka yao katika mapigano ya ndani nchini Burundi.
0 comments:
Post a Comment