UELEWE UHUSIANO WA 'KARIBU' WA JOHN PAUL II NA MWANAMKE
Mamia ya
barua na picha zinazosimulia kuhusu uhusiano wa karibu kati ya Papa John
Paul II na mwanamke aliyeolewa zimeoneshwa kwa BBC.
Urafiki huo ulidumu kwa miaka 30.
Barua
hizo alizomwandikia mwanafalsafa Mmarekani, ambaye ni mzaliwa wa Poland,
Bi Anna-Teresa Tymieniecka zimewekwa faraghani katika Maktaba ya Taifa
ya Poland kwa miaka mingi.
Zinafichua sura nyingine ya maisha ya kiongozi huyo wa kidini, aliyefariki mwaka 2005.
Hata hivyo, hakuna ishara zozote kwamba Papa alikiuka kiapo chake cha useja.
Urafiki
wao ulianza 1973 pale Bi Tymieniecka alipowasiliana na Papa huyo, wakati
huo akiwa Kadinali Karol Wojtyla, aliyekuwa akisimamia Jimbo Kuu la
Krakow, kuhusu kitabu cha filosofia ambacho kiongozi huyo wa kidini
alikuwa amekiandika.
Mwanamke huyo aliyekuwa wakati huo na umri wa miaka 50 alisafiri kutoka Marekani hadi Poland kujadili kitabu hicho.
Baadaye,
wawili hao walianza kuwasiliana. Mwanzoni, barua za kadinali huyo
zilikuwa rasmi, lakini uhusiano wao ulipoendelea kuimarika, zikawa za
undani zaidi.
Wawili
hao walianza kushirikiana katika kuandika upya kitabu cha kadinali huyo
na walikutana mara nyingi, wakati mwingine karani wa kadinali huyo
akiwa, na wakati mwingine peke yao Pia waliwasiliana mara kwa mara.
Mwaka
1974, aliandika kwamba alikuwa akisoma tena na tena barua nne kati ya
alizoandikiwa na Bi Tymieniecka katika mwezi mmoja kwa sababu „zilikuwa
na maana sana na zilikuwa za undani”.
Picha ambazo hazijawahi kuonyesha hadharani kwa umma zinamuonyesha Karol Wojtyla akiwa ametulia sana.
Urafiki
wa Papa John Paul II na Bi Tymieniecka ulianza 1973 Alimwalika Bi
Tymieniecka ajiunge naye katika matembezi na katika likizo akiteleza
kwenye theluji. Wakati mmoja, alijiunga naye katika safari ya kwenda na
kupiga hema. Picha zinaonyesha mwanamke huyo akimtembelea Vatican.
Katika
barua moja Septemba 1976, Kadinali Wojtyla anaandika: "Mpendwa Teresa,
nimepokea barua zote tatu. Unaandika kuhusu kutamauka, lakini sikupata
jibu kuhusu maneno hayo.”
Anamweleza kama “zawadi kutoka kwa Mungu”.
BBC
haijaona barua zozote za Bi Tymieniecka. Lakini inaaminika ziliuziwa
Maktaba ya Taifa ya Poland na Bi Tymieniecka mwaka 2008, miaka sita
kabla yake kufariki.
Lakini hazikuwa pamoja na barua zilizoandikwa na Papa ambazo BBC ilioneshwa.
Kadinali
Wojtyla alikuwa na marafiki kadha wengine wa kike, akiwemo Wanda
Poltawska, mtaalamu wa masuala ya akili ambaye waliwasiliana naye kwa
miongo kadha.
Lakini kwenye barua zake kwa Bi Tymieniecka anaonekana wakati mwingine kuguswa sana n ahata kutatizwa na maana ya uhusiano wao.
Papa John Paul II alifariki 2005, baada ya kuongoza Kanisa Katoliki kwa miaka 27. Mwaka 2014 alitawazwa kuwa mtakatifu.CHANZO:BBC
0 comments:
Post a Comment