VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KABLA YA KUPATA AJIRA RASMI
Afisa
Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma
hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV)
kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez.
Vijana
nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia
ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka
kazi inayoanza na maslahi makubwa.
Hayo
yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma-
Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali
zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.
Bi
Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa
wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini
kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na
kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.
Ameongeza
kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa
pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila
kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo
yanafuata.
“Ukitaka
maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange
nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na
mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,
“Vijana
mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza
kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho
wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Na kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo mengi kwao pia kupata elimu mpya.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana wengi zaidi.
Alisema kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.
Aidha, aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV).
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.
Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), (kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa maelezo kuhusu YUNA inavyofanya kazi kwa jamii ya Tanzania na hususani vijana katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Mkurugenzi Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya kazi katika kuisaidia jamii.
Mmoja wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
Meneja wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Pichani juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni mwa vijana hao.
Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja
0 comments:
Post a Comment