WAHAMAIJI HARAMU 15 KUTOKA ETHIOPIA WAKAMATWA SINGIDA
Idara ya
uhamiaji mkoa wa Singida, imefanikiwa kukamata vijana wahamiaji haramu
15 kutoka nchini Ethiopia, kwa tuhuma ya kuingia na kuishi nchini bila
kuwa na vibali halali.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake juzi,Afisa Uhamiaji mkoa wa
Singida,DCIS Faith Ihano,alisema wahamiaji hao haramu,wamekamatwa
Februari, 12 mwaka huu saa 12.00 jioni Unyankindi mjini hapa.
Alisema
wahamiaji hao wamekamatwa wakiwa wamefichwa kwenye nyumba ya mtu binafsi
Unyankindi mkabala na kota za nyumba za shirika la nyumba taifa (NHC).
“Kwa sasa
tunamshikilia mwenye nyumba huyo kwa mahojiano zaidi na pindi
upelelezi/uchunguzi utakapokamilika,tutamfikisha mahakamani kujibu
tuhuma inayomkabili ya kupokea na kuhifadhi wahamiaji haramu,” alisema
Ihano.
Aidha
Afisa huyo alisema katika kipindi kifupi cha kati ya disemba na januari
mwaka huu,wamefanikiwa kukamata wahamiaji haramu 30 kutoka Congo, Malawi
na Ethiopia.
“Hii
biashara haramu ya kusaidia na kuhifadhi raia wa kigeni wanaoingia
nchini kinyume na taratibu na sheria,inafanywa na Watanzania wachache,”
alifafanua.
Ihano
alitumia fursa hiyo kuwaasa Watanzania wachache wanaojihusisha na
biashara hiyo haramu,kuacha mara moja,vinginevyo
wakibainika,watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa
mujibu wa kijana mmoja Mohammed,ambaye ndiye pekee aliyeweza kuongea kwa
kiingereza cha kubabaisha,alisema wametoka kwao kupitia Kenya na lengo
ni kufika Afrika kusini kusaka maisha bora.
Jumla ya
wahamiaji haramu 15 kutoka Ethiopia (walioketi) wakiwa nje ya ofisi ya
uhamiaji mkoa mjini Singida,jana.Vijana hao walikuwa njiani wakielekea
Afrika kusini kusaka maisha. (Picha na Nathaniel Limu)
Baadhi ya maafisa uhamiaji mkoa wa Singida. |
0 comments:
Post a Comment