WAZIRI MKUU AAGIZA MIANYA YA WIZI WA MAFUTA IDHIBITIWE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mhandisi, Aloys Mtei (kulia) kuhusu mabomba yanayotawanya mafuta kwenda kwenye matangi makubwa ya makampuni mbalimbali kwenye eneo la Kigambo jijini Dar es salaam Februari 11, 2016
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na Wakala wa Vipimo (WMA) kuhakikisha mafuta yanayoingia nchini yanasafirishwa na kupimwa kwa usahihi ili kuiwezesha Serikali kupata kodi sahihi.
Akizungumza wakati wa kukagua mifumo ya upokeaji, usafirishaji na upimaji wa mafuta yanaposhushwa melini Mhe. Majaliwa amesisitiza umuhimu wa taasisi za serikali zinazosimamia suala hilo kufanya kazi kwa umoja ili kuokoa mapato yanayoweza kupotea kwa sababu za wizi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo lenye mabomba yanayotumika kupitisha mafuta kutoka kwenye meli kupitia bandari ya Dar es slaam wakati alipofanya ziara ya kukagua miundombinu yenye mianya ya ukwepaji kodi hasa kwenye mafuta yanayoingia nchini Februari 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Aidha ameagiza mabomba ya kusafirisha mafuta kwenda kwenye matanki yaliyojengwa katika eneo la Kigamboni yasiosimamiwa na TPA yabomolewe katika kipindi cha mwezi mmoja.
“Nakuagiza Msajili wa Hazina vunja mkataba wa ubia kati ya Serikali na kampuni ya ORYX zinazomiliki (TIPPER) ili Serikali iwe na kampuni yake yenyewe itakayopokea na kuhifadhi mafuta badala ya iliyopo sasa ya TIPPER inayoendeshwa kwa ubia.
Ameagiza kuanzia sasa utaratibu wote wa kusafirisha mafuta kutoka katika meli kwenda kwenye matanki kwa wafanyabiashara wote usimamiwe na TPA.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua flow Meter ya Mafuta ya kupikia ambayo
matumizi yake yalizuiwa na Wakala wa Vipimo na Mizani kwa madai kuwa
ilikuwa na kasoro. Wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo na
Mizani, Magdalen Chuwa.
Kwa
upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa amemhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa kuwa TPA imejipanga vizuri
kuhakikisha mafuta yanayoingia nchini yanasafirishwa na kupimwa kwa
usahihi ili Serikali ipate kodi stahili na imejenga mtambo mpya eneo la
Kigamboni utakaosafirisha na kupima mafuta yote utakaoanza kazi mwezi
Machi, 2016.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa ametembelea Chuo cha Mabaharia cha
Dar es salaam (DMI), na kusisitiza umuhimu wa chuo hicho kuongeza fursa
za wanafunzi na walimu ili kuvutia watu wengi kusoma masomo ya ubaharia
na huduma za meli.
Prof.
Mbarawa amemwagiza Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Eng. Yassin Songoro kutafuta
wabia wazuri watakaowezesha chuo hicho kujenga majengo ya kisasa
yanayoendana na mitambo ya kisasa iliyopo ya kufundishia.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Vipimo na Mizani, Bibi Magdalena Chuwa (kulia) kuhusu sababu
zilizomfanya azuie matumizi ya flow Meter katika kuhakiki kiwango cha
mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es salaam wakati
alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Februari 11, 2016.
“Mnayo
mitambo mizuri ya kufundishia hivyo ongezeni fursa za wanafunzi na
walimu ili sekta ya huduma za meli na ubaharia nchini ipate wataalam
wengi na kukuza uchumi wa chuo chenu na taifa”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha
amekitaka chuo hicho kuwa na uhusiano mwema na vyuo vya aina hiyo
duniani ili kubadilishana uzoefu katika mafunzo na kunufaika
kimiundombinu na kitaaluma.
Waziri
Mbarawa amesisitiza umuhimu wa kutangaza kozi zinazotolewa chuoni hapo
na faida zake ili kuwavutia vijana wengi kusoma taaluma za meli na
bahari.
Chuo cha
Mabaharia DMI kilichiopo Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1991 kwa
sheria namba 22 ya Bunge na kinatoa kozi za msingi kuhusu usafiri wa
majini na uhandisi wa meli katika ngazi za cheti, stashahada na shahada.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Wazri
Mkuu,Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujezi na Uchukuzi, Profesa Makame
Mbarawa (kulia) wakimsikiliza Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania, Mhandisi, Aloys Mtei wakati alipotoa maelezo kuhusu uingizaji
wa mafuta kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es salaam Februari
11, 2016.Mheshimiwa Majliwa alikuwa katika ziara ya kukagua miundombinu
yenye mianya ya ukwepaji kodi kwenye mafuta yanayoingia nchini kupitia
bandari hiyo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
bandari Tanzania, Mhandisi Aloys Mtei eneo zinakotia nanga meli kubwa
zinazoleta mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es salaam Februari 11,
2016.
WaziriMkuu,
Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Flow Meter eneo la Kigamboni jijini
Dar es salaam Februari 11, 2016. Mtambo huo utatumika kupima wingi wa
mafuta yanayotoka kwenye meli na kuingizwa hapa nchini. Kulia kwake ni
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymound Mushi.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment