ZIKA YAFANYIWA UTAFITI NCHINI BRAZIL KUHUSU
Wanasayansi wa Marekani wanachunguza uhusiano kati ya virusi vya Zika na hali ya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo
Wanasayansi
kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa CDC nchini Marekani
wameanza kufaya utafiti nchini Brazil ili kujua uhusiano kati ya Virusi
vya Zika na watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
Timu za
wanasayansi zimekuwepo katika jimbo la paraeeba,kaskazini magharibi mwa
nchi hiyo, jimbo ambalo limeathirika zaidi na Virusi.
Timu nane
zinazoundwa na cdc na mawakala wa maswala ya afya walienda kwenye
maeneo yaliyoathirika na kuchukua sampuli ya damu na kuwahoji wamama
walioathirika na wamama ambao watoto wao walizaliwa wakiwa na vichwa
vidogo.
Katika
kipindi cha majuma yajayo, watakusanya taarifa kutoka kwa mamia ya
wamama katika jimbo la paraeeba, jimbo la pili lililoathirika zaidi.
Katika
Ripoti ya siku ya jumanne Wizara ya Afya ya Brazil imethibitisha watoto
587 wana vichwa vidogo.asilimia 75 zaidi ya wiki iliyopita huku maelfu
ya watoto wanachunguzwa.
Baada ya
kutangazwa hali ya taadhari ya kiafya, Rais wa Shirika la Afya duniani,
Margaret Chan aliwasili Brasilia kufuatilia hali ilivyo.
Akiwa
huko alikutana Rais wa Brazil,Dilma Roussef siku ya jumanne na kusema
kuwa anafurahishwa na namna Serikali inavyoshughulikia tatizo hilo na
kutaka jamii isaidiwe kupambana na mbu anayeeneza virusi vya Zika.
BBC
0 comments:
Post a Comment