Friday 11 March 2016

EUROPA; LIVERPOOL YALIPA KISASI KWA MANCHESTER UNITED

Sturridge watches on as his effort curls inside the right-hand post of United goalkeeper David de Gea (centre)
LIVERPOOL imejiweka katika nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali ya michuano ya UEFA Europa League, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mahasimu wao, Manchester United Uwanja wa Anfield usiku wa Alhamisi.
United sasa watatakiwa kwenda kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Machi 17 Uwanja wa Old Trafford ili kwenda Robo Fainali.
Katika mchezo huo, bao la kwanza la Liverpool lilifungwa na Daniel Sturridge kwa penalti dakika ya 20, baada ya Nathaniel Clyne kuangushwa na Memphis Depay kwenye boksi.
Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester United usiku huu Uwanja wa Anfield 


Mshambuliaji Mbrazil, Roberto Firmino Barbosa de Oliveira akaongeza matumaini ya Liverpool kwenda Robo Fainali baada ya kufunga bao la pili dakika ya 73.

Klopp and his Liverpool players celebrate at full-time as they defeated United 2-0 in the Europa League first leg

Katika mchezo huo shujaa aliyefanya matokeo hayo kubaki hivyo ni golikipa David De Gea baada ya kuokoa michomo takribani mitatu ambayo ni dhahiri ingezaa mabao kwa Liverpool.
 Mchezo wa marudiano utapigwa wiki ijayo katika uwanja wa Old Traford ambapo ili kusonga mbele Manchester watahitaji ushindi wa goli 3 kwa bila.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA