INDONESIA: SERIKALI YAONYA KUTOKEA KWA TSUNAMI
Maelfu ya
raia wa Indonesia wakifanya ibada katika Msikiti Mkuu wa Banda Aceh
tarehe 26 Desemba 2014, wakiwakumbuka waathirika wa tsunami ya mwaka
2004.
Na RFI
Tetemeko
la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 richter katika Bahari ya Hindi limepiga
Jumatano hii katika kisiwa cha Sumatra magharibi mwa Indonesia, eneo
lililokumbwa na kuharibiwa na tetemeko la ardhi mwaka 2004. Serikali
imetoa onyo kwa kutokea kwa tsunami.
Tetemeko
hili limetokea saa 12:50 jioni saa za Indonesia (sawa na saa 6:50 saa
za kimataifa) kwenye kilomita 24 za kina na kitovu kilikuwa kilomita
kadhaa na visiwa vya Mentawi, eneo dogo kusini magharibi mwa Sumatra,
kitengo cha utabiri wa mambo ya hewa cha Marekani (USGS)kimesema.
USGS, hata hivyo, imesema katika tovuti yake kwamba "uwezekano wa majeruhi na uharibifu"haukua kwa kiwango kikubwa.
Idara ya
utabiri wa hali ya hewa nchini Indonesia (BMKG) imetoa onyo kwa kutokea
tsunami katika sehemu mbalimbali za Sumatra, hususan Sumatra ya
Kaskazini na Sumatra ya Magharibi, pamoja na Aceh, Bengkulu na Lampung.
Mji ulio
karibu na Sumatra ni Padang. Mwandishi wa habari wa Shirika la habari la
Ufaransa la AFP katika mjihuo amearifu kwamba tetemeko kubwa la ardhi
limesikika kwa sekunde chache na wakazi waliondoka haraka katika nyumba
zao.
Tukio hili limesababisha hali ya wasiwasi katika mitaa, kwa mujibu wa chanzo hicho.
Kiongozi
wa Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Indonesia (BMKG), Andi Eka
Sakya, hata hivyo, amesema kwenye televisheni moja nchini humo TV
One: "Kwa sasa hatuna taarifa kuhusu uharibifu mkubwa."
Jinsi tetemeko la ardhi lilivyosababisha tsunami ya 2004.
Kwa
upande wake, Australia pia imetoa onyo kwa kutokea kwa tsunami katika
mikoa ya magharibi ya Nchi-bara, jirani ya Indonesia, lakini baadae onyo
hilo lilifutwa.
Indonesia
iko kwenye "eneo la hatari" la Pasifiki, ambapo mgongano wa mihimili ya
tectonic husababisha matetemeko ya mara kwa mara na mlipuko muhimu wa
volkano.
Mwaka
2004, tetemeko kubwa, kaskazini magharibi mwa Indonesia, lilisababisha
tsunami kubwa, lililoua watu zaidi ya 170,000 nchini Indonesia na mamia
ya maelfu zaidi katika nchi nyingine kadhaa za Bahari ya Hindi.
Tangu tsunami ya mwaka 2004, hatua za kuzuia au kukinga hali hiyo zimechukuliwa duniani kote.
0 comments:
Post a Comment