Sunday 20 March 2016

SOUTHAMPTON YAIDUWAZA LIVERPOOL IKISHINDA 3-2

SAIDIO MANE ACHARUKA NA KUITIBULIA LIVERPOOL MAHESABU

Matumaini ya timu ya Liverpool kutinga katika nafasi tano za juu za msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza yaliingia dosari baada ya Southampton kubadilika ghafla na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika dimba la St Mary's.

Liverpool walionekana kuumudu vyema mchezo huo baada ya Philippe Coutinho na Daniel Sturridge kupachika mabao yakifuatana kwa tofauti ya dakika tano na kuifanya iongoze kwa mabao 2-0.

Lakini Sadio Mane licha ya kukosa penati alijirekebisha na kufunga bao katika dakika ya 64, kabla ya Graziano Pelle kufunga la pili dakika ya 83 na kisha Mane kuandika bao la tatu katika dakika ya 86.
       Golikipa wa Liverpool akiipangua penati iliyopigwa kiuchovu na Sadio Mane
   Sadio Mane akipiga mpira wa kuzungusha uliompita kipa wa Liverpool na kujaa wavuni

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA