Sunday 13 March 2016

TP MAZEMBE YALAZIMISHWA SARE 2-2 LIGI YA MABINGWA



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amehusika katika mabao yote mawili ya TP Mazembe ikilazimishwa sare ya 2-2 na wenyeji St George katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika leo nchini Ethiopia. 
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Bahir Dar nje kidogo ya mji wa Addis Ababa, Ulimwengu alicheza kwa dakika 63 kabla ya kumpisha Rogger Asale.
Akicheza mechi yake ya kwanza baada ya kupona maumivu ya mguu yaliyomuweka nje tangu Januari, Uliwengu alimsetia Daniel Adjei kuifungia bao la kwanza Mazembe dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kutimia.
Na Ulimwengu tena akapiga mpira uliombabatiza mchezaji wa St George, Isaac Isiende na kutinga nyavuni kuipatia Mazembe bao la pili dakika ya 46, yaani mwanzoni tu mwa kipindi cha pili.
Mabao ya St George yamefungwa na Assefa Behailu dakika ya 11 na Girma Adane dakika ya 60 na sasa Mazembe, mabingwa watetezi wa michuano hiyo wanaweza kusonga mbele hata kwa sare ya 0-0 nyumbani Lubumbashi wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA