Sunday 1 May 2016

KILIMANJARO::WASOMI ELIMU YA JUU WAJITOA KUIHUDUMIA JAMII



Baadhi ya wanafunzi hao wakifyeka majani ikiwa ni sehemu ya usafi hospitalini hapo

Jamii imekuwa ikishuhudia wimbi la uhitaji likiongezeka sanjari na kuwepo kwa wasomi wengi ambao nao wameungana na wahitaji kulalamika pasi na kuwa sehemu ya kutatua matatizo hayo. Hii imekuwa tofauti kwa wanafunzi wa Stefano Moshi Memorial University College walioamua kuwa sehemu ya utatuzi wa matatizo kwa kujitoa kuisaidia jamii kwa hali na mali.

Wakiwa katika Hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro "Kamera Yetu" iliwanasa wakiungana kufanya usafi katika mazingira yanayozunguka hospitali hiyo na baada ya hapo kuzuru wodi ya watoto hospitalini hapo.

Wanafunzi hao walipokuwa wakiwasili hospitlini hapo

Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya wanafunzi hao wa wakwanza ,mwaka wa pili na watatu walisema wanajisikia kama sehemu halali ya jamii kwani nao wamethubutu kuonesha namna wanavyoweza kuwa na mchango chanya kwa jamii.

"Binafsi najisikia furaha kwani naamini kama kila mmoja akijitoa kwa kile alichonacho (hata kwa kufanya usafi pekee) dhana ya kuitupia lawama serikali kuwasaidia wasiojiweza itakuwa historia" alisema Mohamed mwanafunzi mwaka wa pili kitivo cha biashara.


Mtandao huu ulitaka kufahamu hasa nini kiliwasukuma kufika hospitalini hapo na kama huo ndio mwisho wa tukio kama hilo walisema kuwa wameunda umoja ambao lengo kuu ni  kujitoa kuihudumia na hivyo hawataishia hapa ila kwa kadiri ya uihitaji watajitahidi kutoa ushirikiano.


Hii siyo mara ya kwanza kwa wasomi kuzuru sehemu yenye wahitaji lakini wengi wamekuwa wakiacha kujitoa kwa jamii pindi wanapomaliza masomo hivyo FUNGUKA LIVE licha ya kuwapongeza kwa kitendo hichi cha UTU kinawasihi isiwe mwisho kwa wasomi kujitoa kuihudumia jamii hata wanapotawanyika baada ya masomo.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA