Saturday 7 May 2016

MANCHESTER UNITED WATAKATA NA KUIDIDIMIZA NORWICH KUELEKEA KUSHUKA DARAJA


Nafasi ya timu ya Norwich City kuepuka kushuka daraja inaonekana kuzidi kuyeyuka baada ya kufungwa nyumbani kwao na Manchester United goli moja kwa bila.

Mchezo huo ulikuwa na nafasi chache mno za kufunga, lakini bahati ilikuwa kwa Manchester United iliyofanikiwa kupata goli moja lililofungwa na Juan Mata.

Hata hivyo kabla ya goli hilo Cameron Jerome, alipata nafasi nzuri sana kwa Norwich kufunga, lakini kipa David de Gea aliokoa mpira huo wa kichwa.
                                             Juan Mata akifunga goli pekee katika mchezo huo
                                      Wayne Rooney akinyanyua mguu juu kutuliza mpira

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA