Tuesday 17 May 2016

NEWS ALERT:KAFULILA ASHINDWA KESI YAKE YA KUPINGA MATOKEO


Aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini, David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima.

Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.

Katika kesi hii upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Hasna) uliongozwa na wakili Kennedy Fungamtama pamoja na Mawakili wa Serikali upande wa mwanasheria mkuu wa Serikali.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA