Monday 23 May 2016

YAJUE HAYA KUHUSU VAN GAAL NA REKODI YAKE KUHUSU MANCHESTER UNITED


Louis Van Gaal  ameiongoza timu hiyo katika  michezo 103  na kuiwezesha kushinda 54 , kutoa suluhu 25 na kupoteza 24.


Louis Van Gaal  ameiwezesha manchester united kutwaa taji la 12 la FA na taji pekee katika michuano hiyo tangu Sir Alex Fergurson alipofanya hivyo mwaka 2004.


Van Gaal ameiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la fa tarehe 21 /05 /2016 na kufukuzwa kazi tarehe 23 / 05 /2016 akwa ameingia kwenye rekodi ya kocha kutimuliwa kazi ndani ya siku mbili tangu awezeshe timu yake kutwaa kikombe.


VanGaal  amepewa £ 5million kama sehemu ya kuvunja mkataba pamoja na £ 400,000 ikiwa ni pesa zinazoambatana na zawadi za ushindi wa kombe la FA.

Manchester united imekuwa klabu ya pili ambapo Van Gaal amepata    mafanikio kiduchu kulinganisha vilabu vyote vitano alivyofundisha na kujizolea vikombe 20 huku kimoja pekee kikiwa kutoka Old Trafford.(Ajax-11), (Barcelona-4), (AZ Alkmaar-1), (Bayern Munich-3).




0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA