EURO 2016: URENO YA CHRISTIANO RONALDO YATULIZWA NA VIBONDE ICELAND
URENO imeanza
vibaya kampeni zake za kusaka taji la Euro 2016 baada ya kulazimishwa sare na
timu isiyopewa nafasi - Iceland. Luis Nani aliifungia Ureno bao la kuongoza
dakika ya 31 lakini Bjarnason akaisawazishia Iceland dakika ya 50 wakati
supastaa wa Ureno Cristiano Ronaldo akipoteza nafasi ya wazi ya kuifungia nchi
yake bao la ushindi.
Nani akishangilia goli lake |
![]() |
Ronaldo akifanya yake wakati akipambana kuibeba timu yake ya taifa |
Ukingoni mwa mchezo, Nani alimtumia Ronaldo krosi tamu akiwa ndani ya sita lakini Ronaldo ambaye anaweza kuwa ndiye mfungaji bora wa magoli ya vichwa barani Ulaya, akaishia kupiga mpira uliokwenda mikononi mwa kipa Hannes Halldorsson.
Vieirinha anaserereka chini baada ya kuukosa
mpira na kuruhusu Bjarnason wa Iceland
afunge kirahisi
Bjarnason
akiruka juu na kushangilia goli la kwanza kwa Iceland katika historia ya
michuano ya Ulaya
0 comments:
Post a Comment