JOSE MOURINHO AMTAKA LIONEL MESSI OLD TRAFFORD
MANCHESTER
United wanaandaa uwezekano wa kufanya uhamisho mkubwa wa kumsajili straika wa
Barcelona, Lionel Messi. Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti kuwa,
United imetuma maombi mara mbili katika wiki tatu zilizopita katika jaribio la
kumsajili Muargentina huyo. Uhamisho wowote unaonekana kulenga kuirejesha
United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya Jose Mourinho msimu wa 2017/18.
Usajili wa Messi
unaweza kuvunja rekodi ya pauni mil 85.3 ambazo Real Madrid walilipa kwa
Tottenham ili kumnasa Gareth Bale. Mkataba wa sasa wa Messi Nou Camp
unatarajiwa kumalizika 2018 na imebainika kuwa anahitaji kuhakikishiwa mambo
kadha kama wanataka kumbakisha Barcelona ambapo amefunga jumla ya mabao 453
katika mechi 531.
United imekuwa ikisaka mchezaji mwenye jina
kubwa na ishajaribu kumsajili Cristiano Ronaldo hivi karibuni, wakati pia
ishajaribu kuwanasa Bale na Neymar mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment