Monday, 20 June 2016

JWTZ YAKANUSHA TAARIFA ZA KUIBWA KWA KIFARU


Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)  limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru  cha jeshi zilizoripotiwa leo na gazeti la Dira  na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowowte huku  likisisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.

Akiongea na  waandishi wa habari leo  kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari hizo za upotoshaji kwa kuwa zinachafua taswira ya jeshi na taifa kwa ujumla.
 
Amelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja na wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
TAZAMA VIDEO

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA