Monday, 20 June 2016

MASANJA MKANDAMIZAJI ARINDIMA KATIKA MKUTANO WA OYES 2016 JIJINI MWANZA

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016
Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akiimba katika Mkutano wa OYES 2016
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (Kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola (Kulia) katika Mkutano wa OYES 2016
Mama Mchungaji, Mercy Kulola (kushoto) akiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Mwimbaji Chamwenyewe Jembe (Kushoto) pamoja na Mhubiri na Mwimbaji Joseph Rwiza (Kulia) wote kutoka mkoani Morogoro wakiwa katika Mkutano wa Injili wa OYES 2016
Wazee wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Ni katika Mkutano wa OYES 2016 ambao umewafungua watu wengi kiroho
Wakazi wa Jiji la Mwanza pamoja na Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016
Wakazi wa Jiji la Mwanza pamoja na Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwa katika Mkutano wa OYES 2016.
Soma HAPA Kuhusu Mkutano wa OYES 2016

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA