Thursday 23 June 2016

KISASI::CHILE YAIFUATA ARGENTINA FAINALI COPA AMERICA


Chile watavaana na Argentina jumapili katika fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuifunga Colombia magoli 2-0 katika mchezo ambao ulichelewa kuanza kwa saa nne kutokana na mvua.
Katika mchezo huo Charles Aranguiz alipachika goli la kwanza kwa mpira uliompita kiga wa Arsenal, David Ospina na kuifanya Chile iongoze na kisha Jose Pedro Fuenzalida kufunga la pili dakika nne baadaye.

Fainali hiyo inajirudia kama ilivyokuwa mwaka jana wakati mataifa hayo yalipokutana katika michuano hiyo na Chile kushinda kwa mikwaju ya penati.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA