Friday 10 June 2016

MAELFU WAMSWALIA MUHAMMAD ALI MWILI KUZIKWA IJUMAA HII

Jeneza lillobeba mwili wa Muhammad Ali

Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza lilobeba mwili wa bondia mashuhuri duniani marehemu Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani. Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.
Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville. Swala hiyo ilirushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba hatua hiyo inaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani. Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana.
Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu. Mazishi yake yatafanyika Ijumaa hii.

Baadhi ya waumini wa Kiislam walioshiriki ibada ya kuuswalia mwili wa Muhammad Ali 

Jeneza lililobeba mwili wa Muhammed Ali likiingizwa msikitini tayari kwa kisomo maalum
   Kaka wa Muhammed Ali, Rhaman Ali akielekea msikitini kuwahi kisomo cha mdogo wake
Mke wa pili wa zamani wa Ali, Khalilah Camacho-Ali (kushoto), akisimama karibu na mke mwenza Lonnie Ali ambaye ni mke wa nne

                   Veronica Porche-Ali (kushoto), mke wa zamani wa Muhammed Ali
             Binti wa Muhammed Ali, Laila Ali akiwa amembeba mtoto wake wa kike

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA