Monday 20 June 2016

MO BEJAIA YAITULIZA YANGA KWA KIPIGO CHA 1 :0

MABINGWA wa Tanzania YANGA ya jijini Dar es Salaam wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji MO Bejaia, mchezo huo ukipigwa kwenye dimba la Unite Maghrebine huko Bejaia.

Bao hilo muhimu kwa Bejaia liliwekwa nyavuni na mlinzi wake Yassine Salhi katika dakika ya 20, baada ya kuzitendea haki jitihada za straika Ismail Belkacemi. 

Yanga walionyesha upinzani mkubwa katika dakika zote za mchezo ingawa mipango yao ya kulifikia lango la wenyeji ilikuwa ikikwamishwa na viungo wa waarabu hao huku mabeki wao wakimalizia kazi nyepesi.

Kupoteza mchezo huu si jambo zuri kwa Yanga kwavile katika hatua ya makundi jambo muhimu zaidi ni kupata pointi tatu na hii tayari ni faida kwa Bejaia walioko nafasi ya pili huku kundi likiongozwa na TP Mazembe  iliyoanza vema michuano hiyo kwa kuitandika Medeama ya Ghana 3-1 kwenye uwanja wa Mazembe jijini  Lubumbashi.

Kundi hilo litakuwa gumu na lisilotabirika kama Yanga inayoshika nafasi ya tatu itaifunga Mazembe kwenye mchezo wao utakaopigwa Juni 28 katika dimba la Taifa jijini Dar na pia Bejaia ikipoteza ugenini dhidi ya Medeama. 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA