Monday, 20 June 2016

EURO 2016::SWITZERLAND ,UFARANSA HAKUNA MBABE WOTE WATINGA 16 BORA


Switzerland na Ufaransa wametoka sare tasa katika mchezo wao wa michuano ya Euro 2016 na kuifanya itinge hatua ya 16, huku Ufaransa ikiongoza katika kundi A.

Katika mabadiliko machache ya kikosi cha Ufaransa ilimtumia Paul Pogba, ambaye alionyesha uhai katika safu ya ushambuliaji ambapo mashuti yake yaligonga mwamba mara mbili.

Mchezaji hatari kwa sasa wa Ufaransa aliyetokea benchi Dimitri Payet pia aligonga mwamba wa goli baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Moussa Sissoko.
                                                         Shuti la Dimitri Payet likigonga mwamba
Paul Pogba akionyesha ujumbe maalum wa Siku ya Baba kwa baba yake aliyekuwa akifuatilia mchezo huo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA