 |
Washindi wa Mr & Miss Talent University mkoa wa Kilimanjaro 2016 wote kutoka chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College |
Na Dickson Mulashani
Usiku wa kuamkia Jumapili mkoa
wa Kilimajaro ulishuhudia shindano la kumsaka mkaka na mrembo mwenye
kipaji kutoka vyuo vikuu mkoani hapa ambapo chuo kikuu cha Stefano Moshi
Memorial University College kiliweza kung'ara kwa kutoa washindi wote wa kwanza
na wakiwa wanafunzi wa shahada ya mawasiliano ya Umma ( Mass Communication).
Katika shindano hilo jumla ya washiriki 36 ambapo 16 walikuwa ni wasichana na 20 walikuwa wavulana
kutoka vyuo vikuu vya Mwenge Catholic University, MOCU ( Ushirika) , KCMC
University, Mweka Wildlife College na Stefano Moshi Memorial
University College (SMMUCo) walichuana vikali katika kuonesha uhodari wa mavazi
na vipaji vyao huku mkali wa muziki Vannessa Mdee akifika kuwapa kampani.
 |
Vannessa Mdee akifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo |
Hongera wana smmuco wenzangu
ReplyDelete