WANACHAMA WA CHAMA CHA WAAJIRI WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO TBL
Kutokana na kampuni ya TBL Group kuonyesha
mafanikio ya kuwa mwekezaji bora nchini na mchango wake kutambuliwa na taasisi
mbalimbali kwa kuitunukia tuzo ,imekuwa kivutio kikubwa kwa taasisi zinazotaka
kupata mafanikio kwa kutembelea viwanda vyake kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu
na kujua siri ya mafanikio.
Wanachama wa Chama cha Waajiri nchini (ATE) wamefanya ziara katika
kiwanda cha TBL cha Ilala ambako wamepatiwa mafunzo ya usalama kazini ikiwemo
kuona uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo.
Wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania(ATE) wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa upishi wa TBL Group Castor Masawe, kuhusiana na uzalishaji wa bia unavyofanyika |
Meneja Usalama,Afya na Mazingira wa TBL Group,Renatus Nyanda aliwapatia
somo la kanuni za usalama zinazotekelezwa na kampuni hiyo ambazo zinalenga
kulinda usalama wa wafanyakazi wanapokuwa kazini na nje ya kazi ikiwemo wageni
mbalimbali wanaofika kiwandani hapo.
Wanachama wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
|
Wanachama hao walifurahishwa na mafunzo hao ikiwemo mkakati
wa kampuni hiyo kuendelea kufanya uwekezaji unaozingatia utunzaji wa
mazingira,kuchangia kuendeleza uchumi wa taifa,kupunguza tatizo la ajira na
kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora.
Baadhi ya wanachama cha Waajiri Nchini (ATE) wakiangalia vikombe vya tuzo mbalimbali ambavyo TBL Group ilishinda |
0 comments:
Post a Comment