Thursday 7 July 2016

EURO 2016:: URENO WATANGULIA PARIS KATIKA FAINALI

Timu ya Wales imejikuta ikishindwa kuweka historia ya kutinga fainali za michuano ya Euro baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-0 kutoka Ureno katika mchezo uliopigwa huko Lyon.

Katika mchezo huo washambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wote walishindwa kutikisa nyavu katika kipindi cha kwanza kilichoishia bila kufungwa goli.

Hata hivyo katika kipindi cha pili Ronaldo aliandika goli la kwanza la mchezo huo kwa mpira wa kichwa katika dakika ya 50, na kuifanya Ureno iongoze.

Wakati Wales na Bale wao wakiwa bado wanatafakari goli hilo, Ronaldo tena aliachia shuti ambalo Luis Nani aliugonga mpira huo na kuandika goli la pili katika dakika ya 53.
Cristiano Ronaldo akiwa juu angani baada ya kuupiga mpira kwa kichwa ambao unaelekea wavuni
      Mpira wa kichwa uliopigwa na Ronaldo ukijaa wavuni na kumshinda kipa wa Wales
Luis Nani akiugonga mpira uliopigwa na Ronaldo na kuubadilisha muelekeo na kuandika goli la pili

PICHA  AFP na REUTERS 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA