KAMPENI YA NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI YAZINDULIWA JIJINI MBEYA
![]() |
Meneja masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe akizungumza na wadau na wasambazaji (hawapo) wa vileo aina ya konyagi kwenye ukumbi wa Hotel ya Beaco Jijini Mbeya |
![]() |
Baadhi ya wasambazaji kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini walishiriki uzinduzi wa Kampeni ya Nunua, Uza Shinda ya Konyagi kwenye Hotel ya Beaco Jijini Mbeya |
Mawakala 2 kujishindia lori la tani
3
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited
(TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii
zake, imezindua kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa
wasambazaji wa bidhaa zake kanda ya Kaskazini.
Kampeni hii inawahusisha
wasambazaji wa bidhaa za TDL nchini kote ilizinduliwa rasmi wiki iliyopita
jijini Dar es Salaam na itadumu kwa muda
wa wiki 12.
Kanda hiyo ya mauzo inajumuisha
mikoa ya Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga
Akizungumza katika uzinduzi wa
kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya
Kibo Palace mjini Arusha mwishoni mwa
wiki, Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe alisema “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL
kuzindua kampeni ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji wa biashara zetu.
Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wa kampeni hii watajishidia magari
mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck). Tunaamini kwa magari haya
wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa utendaji wao ndani ya maeneo yao ya
mauzo”
Pia, kupitia shindano hili tutaweza
kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla. Aliendelea
kusema.
Bwana Kavishe alisema katika shindano hili wasambazaji wa bidhaa za TDL wamewekewa
viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo
kubwa ya kupata mshindi itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa 10. “Tunaamini
kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongezea
chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.
![]() |
Wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo |
0 comments:
Post a Comment