Wednesday 20 July 2016

USAJIL MAJUU:: LIVERPOOL YAMNASA NAHODHA WA ESTONIA, RAGNA KLAVAN

Ragnar Klavan
Picha na LIVERPOOL FC

Timu ya Liverpool yenye maskani yake katika viunga vya Anifield maarufu kama Vijogoo wamefanikiwa kumnsa beki Ragna Klavan kutoka klabu ya FC Augsburg inayoshiriki ligi ya Ujerumani "Bundesliga" kwa ada ya pauni millioni nne katika mkataba wa muda mrefu.
Hii ndiyo namba ya jezi atakayotumia Klavan
Akizungumzia uhamisho huo Klavan amesema hii imekuwa hatua  kubwa na muhimu sana kwani ni heshima kupata fursa kucheza klabu kubwa na yenye mafanikio barani  Ulaya 

"Ndoto yangu iliyodumu kwa miaka 22 ya kucheza katika ligi kuu ya Uingereza sasa imetimia, najipanga kucheza kwa mafanikio" alisema beki huyo mwenye miaka 30.

Klavan anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na kocha  Jürgen Klopp katika majira ya joto kufuatia wachezaji kama Loris Karius, Joel Matip, Sadio Mane and Marko Grujic.

Klopp anaonekana kuwa katika mchakato wa kuunda timu imara na kubwa ili kukabiliana na mikiki ya ligi ambapo atavaana na Arsenal katika uwanja wa Emirate katika mchezo wa ufunguzi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA