TBL KUENDELEA KUFANIKISHA UTOAJI ELIMU YA USALAMA KATIKA JAMII
Kampuni ya TBL Group imetangaza kuwa itaendelea kutoa
elimu ya Usalama katika maeneo yake ya kazi na kwa jamii ili kuhakikisha
matukio ya ajali zisizo za lazima zinapungua hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Usalama kazini wa
kiwanda cha TBL
cha mjini Mwanza,Bw.Method Marco wakati
akielezea mafunzo ya usalama ambayo yamefadhiliwa na kampuni kwa ajili ya
walimu wa shule za msingi na sekondari na wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la
polisi nchini mkoani humo.
SGT Bahati Nzunda akitoa somo kwa walimu wakati wa mafunzo hayo |
Bw.Method alisema linapokuja suala la usalama
na afya haliwahusu wafanyakazi wa kampuni na familia zao tu bali kwa jamii
nzima kwa kuwa wafanyakazi wa TBL Group ni sehemu ya jamii na wanaishi kwenye jamii.
“Sera za kampuni yetu zinahimiza kulipa
kipaumbele mkubwa suala la Usalama na afya sio kwa wafanyakazi tu bali usalama
wa jamii nzima na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kufadhili na
kushiriki katika kampeni mbalimbali za usalama na miradi ya Afya na Mazingira”.Alisema
Marco.
Walimu wakifuatilia mafunzo ya usalama barabarani |
Baadhi ya walimu wakifanya mazoezi katika makundi |
Kuhusiana na ufadhili wa semina ya wakaguzi wa magari kutoka
Jeshi la polisi na
walimu wa shule za
msingi na sekondari alisema kuwa kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na
taasisi hizo kuhusiana na masuala ya usalama hususani kampeni za usalama
barabarani lengo kubwa likiwa ni kupunguza matukio ya ajali nchini.
Kwa upande wa walimu na wanafunzi alisema
kuwa kampuni itaendelea kushirikiana nao ikiwemo wadau wengine kuhakikisha wanapata elimu ya
usalama barabarani “Ukifundisha walimu ni rahisi elimu hii kuwafikia wengi na
wanafunzi wakipata elimu ya awali ya masuala ya usalama na usalama barabarani
wanakua wakiwa na uelewa mpana wa kujikinga na kuchukua tahadhari.
Alisema suala la kuelimisha jamii kuhusiana
na usalama barabarani ni jambo
ambalo kampuni ya TBL Group itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine.
0 comments:
Post a Comment