Sunday 17 July 2016

KUFUATIA JARIBIO LA MAPINDUZI WANAJESHI 2,839 WAKAMATWA UTURUKI

Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amesema wanajeshi 2,839 wakiwemo maafisa wa ngazi za juu, wamekamatwa baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa.

Miongoni mwa wanaoshikiliwa wamo majenerali wawilia wa jeshi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Waziri Mkuu huyo ameliita jaribio hilo la mapinduzi kama doa jeusi katika demokrasia, na kueleza kuwa raia 161 wameuwawa na wengine 1,440 wamejeruhiwa.
Pia Marekani imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameutaka utawala nchini Uturuki kuheshimu sheria wakati wa uchunguzi wao kuhusu mapinduzi hayo.
Kerry amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika mapinduzi hayo inasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa NATO.
Raia wenye hasira wakiwadunda wanajeshi baada ya kuwadhibiti na kuzima jaribio lao la mapinduzi
    Mwanajeshi aliyedhibitiwa na raia akipigwa ngumi nzito ya shavuni na mmoja wa raia

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA