MUUAJI WA POLISI WATANO MAREKANI ALIFANYA TUKIO HILO PEKE YAKE
Micah Johnson, mtuhumiwa anayedaiwa kuwauwa maafisa polisi watano kwa risasi katika maandamano huko Dallas nchini Marekani inasaidikiwa alitenda tukio hilo akiwa peke yake.
Akiongelea tukio hilo lililotokea wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya Wamarekani weusi, Meya Mike Rawlings amesema wanaamini kwa sasa mji wa Dallas upo salama.
Vifaa vya kutengenezea bomu, bunduki aina ya rifle na jarida la kombati vilikutwa nyumbani kwa Johnson ambaye aliwahi kulitumikia jeshi la Marekani nchini Afghanistan.
Johnson ambaye aliuwawa kwa bomu la roboti, kabla ya hapo aliwaambia polisi amechoshwa na mauaji ya watu weusi yanayofanywa na polisi, hivyo analipa kisasi kwa kuwauwa polisi weupe.
Polisi wakitoka na vitu kwenye nyumba ya Micah Johnson
![]() |
Micah Johnson kulia akiwa na kaka yake Tevin na mdogo wao wa kike Nicole |
Aina ya bunduki aliyotumia Micah Johnson kuwadungua kwa risasi polisi
0 comments:
Post a Comment