|
Baadhi ya watoto wanaoishi na kulelewa katika kituo cha Kilimanjaro Orphanage Centre |
|
Wanaumoja wakiwa katika picha ya pamoja katika lango kuu la kuingia chuoni hapo kwa kampasi ya mjini kabla ya kuelekea kituoni |
Umoja wa Kijamii (UKI) ulioanzishwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University wenye lengo la kuitumikia jamii kwa kujitolea kupunguza changamoto za ukali wa maisha katika jamii ulipata fursa ya kukitembelea kituo cha kulea watoto yatima na wenye mahitaji maalum cha Kilimanjaro Orphanage Centre kilichopo kata ya Pasua wilaya ya Moshi mjini mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumzia historia yao, Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Lazaro Edward alisema kituo hicho kinachopokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea kwasasa kinalea watoto wapatao 79 huku watano kati yao wakiwa ni waathirika wa virusi vya Ukimwi kueleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni idadi ya vitanda pamoja udogo wa eneo lakini wanatarajia kukihamisha kituo hicho baada ya ujenzi wa kituo rasmi kukamilika.
|
Wana UKI wakikaribishwa na kupewa maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bw.Lazaro Edward mara tu walipowasili |
Wanaumoja wa UKI wanaosoma kozi mbali mbali walikuwa na wasaha mzuri wa kucheza , kuongea pamoja na kuwakabidhi zawadi watoto hao zenye thamani ya shilingi laki tatu.
Akieleza lengo la kukitembelea kituo hicho mwenyeketi wa umoja huo Bw. Msiyaki Kuruchumila mwanafunzi wa Elimu na Usimamizi wa Bishara alisema kuwa hii ni sehemu ya muendelezo wa majukumu yao kama Umoja wa Kijamii na hivyo bado safari yao kuelekea kujitoa kwa jamii bado ni ndefu.
Mwandishi wetu alipotaka kujua kwanini kuhusu umoja huu kuwa umejikita zaidi katika chuo cha SMMUCo na je yapo malengo zaidi ya kuutanua,Bw. Kuruchumila alisema kuwa wapo katika mchakato wa kuuneza katika vyuo vyote katika mkoa wa Kilimajaro na wanajitahidi hili liwe limekamilika kabla ya mwezi wa kumi na moja mwaka huu. "Sisi kama SMMUCo peke yetu hatuwezi kwa kuwa jamii inamahitaji mengi na baada ya kuridhika kuhusu uimara wetu ndani ya SMMUCo tumeanza mchakato kuhakikisha UKI inasambaa katika vyuo vyote hapa Moshi ikiwa ni MOCu, KCMC,MWECAU na MWEKA" alihitimisha.
|
Wana UKI wakicheza na watoto wa Kilimanjaro Orphanage Centre |
|
Watoto wakiteta jambo huku nyuso zao zikiwa na tabasamu la kutembelewa na wageni |
|
Kulia ni mwenyeketi wa UKI Bw. Msiyaki Kuruchumila akikabidhi zawadi kwa watoto hao |
|
Mwenyekiti wa vijana CCM mkoa wa Kilimanjaro Juma Raibu (Kushoto) akiwa na Rais wa Serikali ya wanafunzi SMMUCo Edgar Nziku ambao wote ni wana UKI wakiwa na watoto kituoni hapo |
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Akizungumzia ziara hiyo mmoja kati ya wanaumoja huo Godilisten Mnuo alisema kuwa amejifunza mambo mengi hasa upendo kutoka kwa watoto hao na kutoa wito kwa wadau mbali mbali kuwa na tamaduni ya kudumisha uhusiano na wenye mahitaji kwa moyo wa dhati katika jamii ili kwani hii ndio sifa bora machoni pa Mungu na wanadamu.
|
Mwana UKI Bw.Said akiwasimulia hadithi watoto |
|
WanaUKI wakiwa wameketi na watoto hao huku wakifuatila masimulizi ya hadithi |
|
Wana UKI wakigawa zawadi kwa watoto |
|
Blogger na muandishi wa mtandao wa Funguka Live Dickson Mulashani ambaye pia ni mwanaumoja wa UKI akifurahia jambo pamoja na watoto hao |
|
Mtoto akipatiwa "juice" na mwanadada amabaye ni mwanaUKI |
|
Afisa habari wa umoja huo Bw. Michael akifuatilia moja hadithi |
|
Baadhi ya kina dada ambao ni wana UKI wakikagua sehemu ya malazi kwa watoto kituoni hapo |
|
Rais wa Serikali ya wanafunzi SMMUCo Edgar Nziku akizungumza na mmoja wa watoto kituoni hapo |
0 comments:
Post a Comment