Friday 1 July 2016

USAJILI LIGI KUU BARA::THEMI FELIX MBIONI KUREJEA KAGERA SUGAR

SIKU tatu baada ya kutangazwa kuachwa na  'Wagonga nyundo' wa jiji la Mbeya, Mbeya City mshambuliaji Themi Felix 'Mnyama' ameibukia kwa wakata miwa wa Kagera Sugar na muda wowote kuanzia sasa atasaini kandarasi na wanankulukumbi hao ambao tayari wameshamalizana na Edward Christopher.


Themi aliwahi kuwa mshambuliaji tishio miaka mitatu iliyopita akiwa na Kagera kabla ya kuhamia City ambapo kiwango kilishuka na sasa anategemea kurudi nyumbani kuendelea kufanya mambo makubwa.

Wachezaji wengine ambao wameshamwaga wino kuwatumikia wakata miwa hao ni David Burhan, Matogolo Anthony na Hassani Khateeb.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA