AGUERO ,NOLITO WAIDIDIMIZA STOKE CITY UGENINI
Washambuliaji Sergio Aguero na Nolito wametikisa nyavu mara mbili kila mmoja wakati Manchester City ikiichakaza Stoke City kwa magoli 4-1 na kuendeleza ushindi wakiwa na kocha Pep Guardiola.
Manchester City walianza kuongoza kufunga kwa mkwaju wa penati, licha ya kukosa penati mbili jumanne, na kuongeza la pili kwa kuunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Kevin de Bruyne.
Bojan aliifungia goli la penati Stoke City katika dakika ya 49 baada ya Raheem Sterling kumchezea rafu Ryan Shawcross hata hivyo Nalito alikuja kufunga magoli mawili katika dakika za mwisho na kukamilisha ushindi.
Sergio Aguero akiifungia Manchester City goli la kwanza kwa mkwaju wa penati
Bojan akiifungia Stoke City goli pekee la timu hiyo kwa mpira wa penati
Nalito akiifungia Manchester City moja ya magoli kati ya mawili aliyofunga
0 comments:
Post a Comment