Saturday 20 August 2016

KUU YA UINGEREZA: MANCHESTER UNITED YAWAPA RAHA MASHABIKI OLD TRAFORD KWA USHINDI


Zlatan Ibrahimovic ametikisa nyavu mara mbili na kuipa ushindi wa nyumbani Manchester United wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Mshambuliaji huyo hatari raia wa Sweden aliwanyanyua mashabiki wa Manchester United katika dimba la Old Trafford baada ya kuupiga kichwa mpira wa krosi iliyopigwa na Wayne Rooney na kuandika goli la kwanza.

Ibrahimovic alifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Jordy Clasie kumuangusha beki wa Manchester United Luke Shaw. Paul Pogba aliyevunja rekodi ya uhamisho wa paundi milioni 89 alicheza kwa mara ya kwanza na kuonyesha uwezo wake.
Ibrahimovic na Paul Pogba wakiangalia mpira wa kichwa ukielekea wavuni na kuipatia Manchester United goli la kwanza
 Zlatan Ibrahimovic akijipinda kuachia shuti la mpira wa penati uliojaa wavuni na kuandika goli la pili

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA